Posts

Showing posts from February, 2017

Batuli akanusha madai ya Wema Sepetu kuidai CCM

Image
Muigizaji wa filamu nchini, Yobnesh Yussuf maarufu kama Batuli amekanusha taarifa iliyotolewa na Wema Sepetu kuwa CCM haijawalipa pesa za kampeni ya Mama Ongea na Mwanao kwenye uchaguzi wa mwaka 2015. Akizungumza na wanahabari kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Protea, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ akiwa na Ndumbangwe Misayo ‘Thea’,amesema madai aliyoyatoa Wema Sepetu hayana ukweli wowote kwa sababu wasanii wote walilipwa. “Nikiwa kama makamu mwenyekiti wa group hili la Mama Ongea na Mwanao kwa muda ni kweli inasemekana kwenye mitandao kuwa tulifanya kampeni na hatukulipwa, mimi kama mwenyekiti msaidizi wa muda nakanusha taarifa hizo kuwa si za kweli. Ingawa kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani,wapo wanaoshawishiwa kulichafua kundi letu, kumchafua Makamu wa Rais Bi Samia Suluhu na kuichafua CCM, mimi nakataa, sote tumelipwa na mikataba ipo, haiwezekani we staa mkubwa unakaa kwenye media unaongea uongo kwamba wasanii hatujalipwa.” Ameongeza, “Zipo simu za kutushawishi kuhama lakini hat...

CHADEMA yaweka ulinzi mkali kwa Mama Wema, ni baada ya nyumba yake kupigwa mawe

Image
Usiku wa kuamkia jana nyumba ya mama mzazi Miss Tanzania, 2006 Wema Sepetu, Mariam Sepetu, imepigwa mawe juu ya bati kwa muda wa saa moja na nusu. Nyumba hiyo ipo maeneo ya Sinza Mori jijini Dar es Salaam. Akizungumza nyumbani kwake Jumatatu hii, Mama Sepetu alisema kuwa usiku wote huo alikosa raha na kupata hofu kubwa na kuhisi kuna watu wabaya waliokuwa wanataka kumvamia. Alisema, “Nimekosa usingizi na hofu juu huku simu yangu iliishiwa salio kwani nilikuwa nikitaka kupigia simu ndugu na majirani ili waje kunisaidia, sikuweza kutoka nje kwa kuwa sikuwa najua mbaya wangu amekaa wapi na amekusudia kufanya nini.” Aidha mama huyo alisema kulivyopambazuka alitoa taarifa kwa mwanae Wema na viongozi wengine wa Chadema ambapo Meya wa Ubungo, Boniface Jacob alifika ili kuangalia hali ya mama huyo na kuamua kumwekea ulinzi. “Tumeshaangalia mazingira yote tumegundua kitu ambacho hatutakiweka wazi kwa sasa ila tutaweka ulinzi mkali na atakayejaribu shauri yake hatutakubali suala hili ...

Adama Barrow amtimua kazi mkuu wa majeshi Gambia

Image
Rais wa Gambia Adama Barrow amemuachisha kazi mkuu wa majeshi wa nchi hiyo Ousman Badjie. Hatua hiyo ya Rais Barrow imekuja kutokana na Badjie kutangaza mwezi Disemba mwaka jana baada ya uchaguzi mkuu kuwa atafuata amri ya Rais aliyepita Yahya Jammeh ambaye alishindwa katika uchaguzi huo. Hata hivyo wanajeshi wa Gambia hawakuweza kutii amri kutoka kwa mkuu huyo wa majeshi ambaye alikuwa chini ya Jammeh ambaye baada ya muda alikubali kuachia madaraka hayo na kukimbilia nchini Equatorial Guinea. Na sasa Masanneh Kinteh ambaye aliwahi kufanya kazi nchini Cuba anachukua nafasi hiyo ya Badjie. Baada ya kuteuliwa katika nafasi hiyo, Kinteh alitaja jambo lake la kwanza ambalo atalifanya katika jeshi lake ni kuwafaja wajiamini ili waongeze hamasa yao. “My immediate priority as chief of defence staff is to bring back the confidence in the troops to lift their morale,” amesema Kinteh.

Mkuu wa shule ajinyonga, yadaiwa chanzo ni upweke

Image
Mkuu wa Shule ya Sekondari Tumuli katika Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida, Richard Makala (58) amejinyonga kwa kamba kutokana na kile kinachodhaniwa ni upweke. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba, amesema mjini Singida kuwa Mkamala alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba iliyotengenezwa kwa vipande vya chandarua iliyofungwa juu ya mti umbali wa mita 130 kutoka nyumbani kwake. Aidha kamanda huyo alisema chanzo cha tukio hilo hakijajulikana na kwamba hakuna mtu au watu wanaoshikiliwa kutokana na tukio hilo na kuongeza kuwa polisi inaendelea na upelelezi kubaini kilichomsibu mwalimu huyo. Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya shule hiyo, Mabruki Ng’ui ameliambia  gazeti la Habarileo  Jumatatu hii kuwa mwalimu huyo alikuwa anaishi peke yake kwa muda mrefu baada ya mkewe ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Tanzania (KKKT) Kitusha wilayani Iramba kuamua kutengana naye kutokana na unywaji pombe. “Huyu bwana amekuwa kwenye ndoa ya j...

Huu ndio ujumbe wa Haji Manara kwa Ramadhani Kessy wa Yanga

Image
Baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga wikiendi iliyopita, Afisa habari wa klabu ya soka ya Simba, Haji Manara amemtumia ujumbe beki wa zamani wa klabu hiyo Hassan Ramadhani Kessy ambaye kwa sasa anacheza Yanga. Kupitia mtandao wa Instagram, Haji ameweka picha ya mchezaji huyo na kuandika, “Unakumbuka Yale maneno aliotudhalilisha huyo dogo?mwambieni THIS IS SIMBA,,na benchi ndio makazi yako ya kudumu.” Kessy alisajiliwa na Yanga akitokea Simba mwishoni mwa msimu uliopita huku usajili wake ukizua utata mkubwa baada ya klabu hiyo ya Jangwani kuonekana kutofuata taratibu za usajili wa mchezaji huyo wakati akiwa bado ana mkataba na Simba ambapo waliamuriwa na TFF kulipa kiasi cha shilingi milioni 50 kutokana na tatizo hilo. Kessy amekuwa na wakati mgumu ndani ya Yanga kwa kukosa namba katika kikosi cha kwanza huku nafasi yake ikichukuliwa na Juma Abdul ambaye yupo kwenye kiwango kizuri kwa sasa.

Wizara ya Maliasili na utalii yafungua rasmi ofisi zake Dodoma

Image
Wizara ya Maliasili na utalii inautaarifu umma kuwa awamu ya kwanza ya watumishi 52 wa wizara ikiongozwa na waziri wake imeanza rasmi kazi kwenye ofisi zake mjini Dodoma. Hii ni taarifa yake:

Ntamshtaki Makonda kwa Mungu na majibu yatapatikana – Gwajima

Image
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ameendelea kuonyesha msimamo wake wa kumshtaki Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa Rais Magufuli huku akidai endapo ataona hakuna hatua inayochukuliwa atamshtaki kwa Mungu na majibu yatapatikana. Askofu Gwajima aliyasema hayo Jumapili hii wakati akiongoza ibada ya Jumapili kanisani kwake Ubungo Maji. “Watu wananiuliza, nitamfungulia kesi. “Mimi nawaambia nitamwambia Rais Magufuli kama nilivyosema, kama hakuna kitu kitakachofanyika basi nitamwambia Mungu aliye juu na majibu yatapatikana,” alisema Askofu Gwajima. Aidha Askofu huyo alisema yeye alipochokozwa haikuwa bahati mbaya ila alidai wanaomchokoza ni sawa na kufungulia koki ya maji yenye mgandamizo mkubwa au wamebusu transfoma ya umeme ambayo ni hatari kwa maisha ya binadamu kuisogelea kama huna utaalamu nayo kwa sababu husababisha kifo. Hata hivyo Askofu huyo alitoa mstari uliopo kwenye biblia ambao ni Yeremia 22: 11 ambapo alisema kila jambo linatokea kwasa...

Ridhiwani aeleza alichoteta na Lowassa Dar

Image
Picha inayomuonyesha waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiteta jambo na Ridhiwani, mtoto wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete imemfanya mbunge huyo wa Chalinze kujitokeza na kuizungumzia Lakini yapo matukio mengi yanayoonyesha “siasa si uhasama” kama alivyosema Ridhiwani, Mwananchi imezungumza na Ridhiwani kuhusu walichoteta na Lowassa na pia inakurejeshea kumbukumbu za wanasiasa walionekana kuwa na uadui, lakini nje ya jukwaa wanaelewana. Picha ya Ridhiwani na Lowassa ilipigwa wakati wa mechi ya watani wa jadi katika soka nchini, Simba na Yanga iliyofanyika Uwanja wa Taifa Jumamosi iliyopita na kuhudhuriwa na maelfu ya watu, wakiwamo wanasiasa ambao walikaa jukwaa kuu na kubadilishana mawazo bila kujali tofauti zao. Katika picha hiyo, Ridhiwani, akiwa amevalia fulana ya njano anaonekana akiwa amemuinamia Lowassa ambaye amekaa, wakionekana kuteta jambo huku wameshikana mkono. Wote wawili wanaonekana kutabasamu. Wawili hao walionekana kuwa na uadui mkubwa ...

Leicester City waanza safari, waichapa Liverpool bila huruma

Image
Klabu ya soka ya Leicester City imefanikiwa kupanda hadi nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuifunga Liverpool kwa mabao 3-1 usiku wa Jumatatu hii. Magoli ya mabingwa hao watetezi wa kombe hilo yalifungwa na Jamie Vard aliyefunga magoli mawili kwenye dakika ya 28 na 60, Danny Drinkwater dakika ya 68 na goli la kufutia machozi la Liver lilifungwa na Philippe Coutinho dakika ya 68. Huo umekuwa ni mchezo wa kwanza wa Leicester kushinda wakiwa chini ya kocha wao mpya wa muda Craig Shakespeare ambaye amekalia kiti hicho baadaya Claudio Ranieri kutimuliwa wiki iliyopita. Liverpool ambao wanashika nafasi ya tano kwenye ligi kuu walikuwa na nafasi kubwa ya kupanda hadi kwenye nafasi ya tatu iwapo wangeweza kushinda mechi hiyo.

SHULE 22 ZAPATIWA MSAADA WA VITABU WILAYA YA KILOLO

Image
 Afisa Miradi wa CAMFED Tanzania, Christina Kyaruzi akizungumza na baadhi ya wakuu wa shule za sekondari zilizoko katika wilaya ya kilolo baada ya kukabidhi vitabu katika shule hizo. Kushoto kwake Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Ilula   Afisa Miradi wa CAMFED Tanzania, Christina Kyaruzi akionyesha moja ya vitabu ambavyo amekibadhi kwa shule 22 za wilaya ya Kilolo halfa zilizofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Ilula.   Afisa Miradi wa CAMFED Tanzania, Christina Kyaruzi akimkabidhi Mwenyekiti Huduma za Jamii wa Halmashauri ya wilaya Kilolo, Anna Kulanga moja ya mfano wa vitabu walivyokabidhi katika shule za sekondari wilaya ya Njombe.   Afisa Miradi wa CAMFED Tanzania, Christina Kyaruzi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ilula.   Afisa Miradi wa CAMFED Tanzania, Christina Kyaruzi mwenye nguo ya njano akiwa na walimu wa shule za sekondari zilizopatiwa msaada wa vitabu kutoka shirika...

IFAHAMU VIZURI WILAYYA YA KILOLO IRINGA

Image
Kilolo ni moja ya wilaya nne za mkoa wa Iringa.Inapakana na Morogoro upande wa kaskazini mashariki, kusini na wilaya ya Mufindi na magharibi ni wilaya ya Iringa vijijini. Kutokana na sensa ya mwaka 2012 ya kitaifa Tanzania, Kilolo ilikuwa na watu wapatao 205,081. Kisiasa Kwa uchaguzi wa wabunge, Tanzania imegawanywa katika majimbo ya uchaguzi. Kwa uchaguzi wa mwaka 2015 wilaya ya Kilolo ina jimbo moja tu, nalo linaitwa Kilolo. Tarafa Wilaya ya Kilolo ina jumla ya Tarafa 4, nazo ni: 1. Mazombe 2. Mtandika 3. Kilolo 4.Ukwega Kata Kwa sensa ya 2012, Wilaya ya Kilolo iligawanywa katika kata zifuatazo,ila zimeongezeka zingine sizifahamu vema, anayejua aongeze kwenye maoni nami nitaziingiza, vile vile na Tarafa. kata hizo ni: Bagamoyo Boma la ng'ombe Dabaga Idete Ilula Nyalumbu Image Irole Mahenge Mtitu Udekwa Uhambingeto Ukumbi Ukwega Ibumu Vijiji  Wilaya inavijiji zaidi ya 100. Kiuchumi Wananchi wa Kilolo asilimia 90 ni wakulima wa mazao mbalimbali ambayo ...