CHADEMA yaweka ulinzi mkali kwa Mama Wema, ni baada ya nyumba yake kupigwa mawe
Usiku wa kuamkia jana nyumba ya mama mzazi Miss Tanzania, 2006 Wema Sepetu, Mariam Sepetu, imepigwa mawe juu ya bati kwa muda wa saa moja na nusu. Nyumba hiyo ipo maeneo ya Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
Akizungumza nyumbani kwake Jumatatu hii, Mama Sepetu alisema kuwa usiku wote huo alikosa raha na kupata hofu kubwa na kuhisi kuna watu wabaya waliokuwa wanataka kumvamia.
Alisema, “Nimekosa usingizi na hofu juu huku simu yangu iliishiwa salio kwani nilikuwa nikitaka kupigia simu ndugu na majirani ili waje kunisaidia, sikuweza kutoka nje kwa kuwa sikuwa najua mbaya wangu amekaa wapi na amekusudia kufanya nini.”
Aidha mama huyo alisema kulivyopambazuka alitoa taarifa kwa mwanae Wema na viongozi wengine wa Chadema ambapo Meya wa Ubungo, Boniface Jacob alifika ili kuangalia hali ya mama huyo na kuamua kumwekea ulinzi.
“Tumeshaangalia mazingira yote tumegundua kitu ambacho hatutakiweka wazi kwa sasa ila tutaweka ulinzi mkali na atakayejaribu shauri yake hatutakubali suala hili liendelee kumkuta kamanda wetu na mimi mara kwa mara nitafika kuangalia mazingira,” alisema Jacob.
Comments
Post a Comment