IFAHAMU VIZURI WILAYYA YA KILOLO IRINGA

Kilolo ni moja ya wilaya nne za mkoa wa Iringa.Inapakana na Morogoro upande wa kaskazini mashariki, kusini na wilaya ya Mufindi na magharibi ni wilaya ya Iringa vijijini. Kutokana na sensa ya mwaka 2012 ya kitaifa Tanzania, Kilolo ilikuwa na watu wapatao 205,081.

Kisiasa

Kwa uchaguzi wa wabunge, Tanzania imegawanywa katika majimbo ya uchaguzi. Kwa uchaguzi wa mwaka 2015 wilaya ya Kilolo ina jimbo moja tu, nalo linaitwa Kilolo.

Tarafa

Wilaya ya Kilolo ina jumla ya Tarafa 4, nazo ni:
1. Mazombe
2. Mtandika
3. Kilolo
4.Ukwega

Kata

Kwa sensa ya 2012, Wilaya ya Kilolo iligawanywa katika kata zifuatazo,ila zimeongezeka zingine sizifahamu vema, anayejua aongeze kwenye maoni nami nitaziingiza, vile vile na Tarafa. kata hizo ni:
  • Bagamoyo
  • Boma la ng'ombe
  • Dabaga
  • Idete
  • Ilula
  • Nyalumbu
  • Image
  • Irole
  • Mahenge
  • Mtitu
  • Udekwa
  • Uhambingeto
  • Ukumbi
  • Ukwega
  • Ibumu
Vijiji
 Wilaya inavijiji zaidi ya 100.

Kiuchumi
Wananchi wa Kilolo asilimia 90 ni wakulima wa mazao mbalimbali ambayo ndiyo haswa tegemeo lao la uchumi, wanalima miti ya mbao, viazi, njegere, mahindi, maharagwe na nyanya ikiwa ni mazao ya biashara na chakula pia.

Kielimu
Kiujumla wilaya haiko katika hali nzuri kielimu, ingawa kuna shule 106 za msingi na zaidi ya 20 za sekondari na vyuo vya kati kama 10 hivi vingi vikiwa na wanafunzi wote toka nje ya wilaya. Wilaya mara nyingi inashika nafasi ya mwisho kimkoa kwa matokeo ya darasa la saba ambao ndiyo msingi wa elimu kuelekea mbele. Inahitajika mawazo mapya na juhudi za kuondoa mazoea na kuhakikisha tunainua kiwangi cha elimu kwa wilaya hii.

Kiafya
Wilaya ya kilolo bado haijajenga hospitali yake ya wilaya, mpaka sasa inatumia hospitali ya kanisa kama teule ya wilaya, hilo linaonyesha kuwa hatukoserous na afya za watu kuwa na hospitali moja wilaya nzima ambayo jiografia yake ni mbaya mno. siyo hospitali rafiki kabisa kwa vijiji husika vilivyo vingi ndani ya wilaya.Vijiji vingi havina hata zahanati ya huduma ya kwanza, vile vyenye zahanati hakuna tabibu wa afya na zahanati yenyewe siyo ya serikali.

Maji
Maji ni uhai, wilaya ya kilolo ina maji kwa baadhi ya kata hasa ya Udekwa,Image na Upande wa Dabaga. lakini ni kero ya miaka nenda rudi kwa wakazi wa Tarafa ya Mtandika na kata ya Ilula. Kwa karne hii tunategemea angalu asilimia 60 vijiji viwe na maji na 85 mijini kuwe na maji.

Barabara
Kwaujumla barabara za vijijini ni mbaya mno hasa kipindi cha masika, viwango ambavyo huwa watengenezea hizo barabara ni vya hali ya chini sana, kama wilaya kunahitajika mkakati wa hali ya juu kuondoa changamoto hiyo. ili kuleta maendeleo ya hima kwa wana wilaya.

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa shule ajinyonga, yadaiwa chanzo ni upweke