Batuli akanusha madai ya Wema Sepetu kuidai CCM

Muigizaji wa filamu nchini, Yobnesh Yussuf maarufu kama Batuli amekanusha taarifa iliyotolewa na Wema Sepetu kuwa CCM haijawalipa pesa za kampeni ya Mama Ongea na Mwanao kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.
Akizungumza na wanahabari kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Protea, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ akiwa na Ndumbangwe Misayo ‘Thea’,amesema madai aliyoyatoa Wema Sepetu hayana ukweli wowote kwa sababu wasanii wote walilipwa.
“Nikiwa kama makamu mwenyekiti wa group hili la Mama Ongea na Mwanao kwa muda ni kweli inasemekana kwenye mitandao kuwa tulifanya kampeni na hatukulipwa, mimi kama mwenyekiti msaidizi wa muda nakanusha taarifa hizo kuwa si za kweli. Ingawa kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani,wapo wanaoshawishiwa kulichafua kundi letu, kumchafua Makamu wa Rais Bi Samia Suluhu na kuichafua CCM, mimi nakataa, sote tumelipwa na mikataba ipo, haiwezekani we staa mkubwa unakaa kwenye media unaongea uongo kwamba wasanii hatujalipwa.”
Ameongeza, “Zipo simu za kutushawishi kuhama lakini hatutohama chama na kundi la Mama Ongea na Mwanao litaendelea kuwepo chini ya Usimamizi wa Bi Samia Suluhu.”

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa shule ajinyonga, yadaiwa chanzo ni upweke