Huu ndio ujumbe wa Haji Manara kwa Ramadhani Kessy wa Yanga

Baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga wikiendi iliyopita, Afisa habari wa klabu ya soka ya Simba, Haji Manara amemtumia ujumbe beki wa zamani wa klabu hiyo Hassan Ramadhani Kessy ambaye kwa sasa anacheza Yanga.
Kupitia mtandao wa Instagram, Haji ameweka picha ya mchezaji huyo na kuandika, “Unakumbuka Yale maneno aliotudhalilisha huyo dogo?mwambieni THIS IS SIMBA,,na benchi ndio makazi yako ya kudumu.”
Kessy alisajiliwa na Yanga akitokea Simba mwishoni mwa msimu uliopita huku usajili wake ukizua utata mkubwa baada ya klabu hiyo ya Jangwani kuonekana kutofuata taratibu za usajili wa mchezaji huyo wakati akiwa bado ana mkataba na Simba ambapo waliamuriwa na TFF kulipa kiasi cha shilingi milioni 50 kutokana na tatizo hilo.
Kessy amekuwa na wakati mgumu ndani ya Yanga kwa kukosa namba katika kikosi cha kwanza huku nafasi yake ikichukuliwa na Juma Abdul ambaye yupo kwenye kiwango kizuri kwa sasa.

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa shule ajinyonga, yadaiwa chanzo ni upweke