Leicester City waanza safari, waichapa Liverpool bila huruma
Klabu ya soka ya Leicester City imefanikiwa kupanda hadi nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuifunga Liverpool kwa mabao 3-1 usiku wa Jumatatu hii.
Magoli ya mabingwa hao watetezi wa kombe hilo yalifungwa na Jamie Vard aliyefunga magoli mawili kwenye dakika ya 28 na 60, Danny Drinkwater dakika ya 68 na goli la kufutia machozi la Liver lilifungwa na Philippe Coutinho dakika ya 68.
Huo umekuwa ni mchezo wa kwanza wa Leicester kushinda wakiwa chini ya kocha wao mpya wa muda Craig Shakespeare ambaye amekalia kiti hicho baadaya Claudio Ranieri kutimuliwa wiki iliyopita.
Liverpool ambao wanashika nafasi ya tano kwenye ligi kuu walikuwa na nafasi kubwa ya kupanda hadi kwenye nafasi ya tatu iwapo wangeweza kushinda mechi hiyo.
Comments
Post a Comment