Ntamshtaki Makonda kwa Mungu na majibu yatapatikana – Gwajima

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ameendelea kuonyesha msimamo wake wa kumshtaki Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa Rais Magufuli huku akidai endapo ataona hakuna hatua inayochukuliwa atamshtaki kwa Mungu na majibu yatapatikana.
Askofu Gwajima aliyasema hayo Jumapili hii wakati akiongoza ibada ya Jumapili kanisani kwake Ubungo Maji. “Watu wananiuliza, nitamfungulia kesi. “Mimi nawaambia nitamwambia Rais Magufuli kama nilivyosema, kama hakuna kitu kitakachofanyika basi nitamwambia Mungu aliye juu na majibu yatapatikana,” alisema Askofu Gwajima.
Aidha Askofu huyo alisema yeye alipochokozwa haikuwa bahati mbaya ila alidai wanaomchokoza ni sawa na kufungulia koki ya maji yenye mgandamizo mkubwa au wamebusu transfoma ya umeme ambayo ni hatari kwa maisha ya binadamu kuisogelea kama huna utaalamu nayo kwa sababu husababisha kifo.
Hata hivyo Askofu huyo alitoa mstari uliopo kwenye biblia ambao ni Yeremia 22: 11 ambapo alisema kila jambo linatokea kwasababu maalum sio kwa bahati mbaya.

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa shule ajinyonga, yadaiwa chanzo ni upweke