Utayarishaji wa filamu ya Avatar 2 kuanza mwaka huu
Muendelezo wa filamu yenye mafanikio makubwa ya James Cameron, Avatar umeanza kunukia. Kwa mujibu wa The Hollywood Reporter, utayarishaji wa Avatar 2 utaanza kufanyika miezi michache ijayo.
Muingozaji na mtayarishaji wake, James Cameron alisema kuwa hatimaye yuko tayari kuanza kuisuka baada ya kumaliza kupanga zingine tatu zinazofuata baada ya hapo.
Waigizaji Zoe Saldana na Sam Worthington wanarejea kama waigizaji wakuu. Filamu ya kwanza ya Avatar ilitoka mwaka 2009. Bajeti yake ilikuwa dola milioni 237 lakini hadi sasa imeingiza dola bilioni 2.788.
Comments
Post a Comment