Mkuu wa shule ajinyonga, yadaiwa chanzo ni upweke
Mkuu wa Shule ya Sekondari Tumuli katika Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida, Richard Makala (58) amejinyonga kwa kamba kutokana na kile kinachodhaniwa ni upweke. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba, amesema mjini Singida kuwa Mkamala alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba iliyotengenezwa kwa vipande vya chandarua iliyofungwa juu ya mti umbali wa mita 130 kutoka nyumbani kwake. Aidha kamanda huyo alisema chanzo cha tukio hilo hakijajulikana na kwamba hakuna mtu au watu wanaoshikiliwa kutokana na tukio hilo na kuongeza kuwa polisi inaendelea na upelelezi kubaini kilichomsibu mwalimu huyo. Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya shule hiyo, Mabruki Ng’ui ameliambia gazeti la Habarileo Jumatatu hii kuwa mwalimu huyo alikuwa anaishi peke yake kwa muda mrefu baada ya mkewe ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Tanzania (KKKT) Kitusha wilayani Iramba kuamua kutengana naye kutokana na unywaji pombe. “Huyu bwana amekuwa kwenye ndoa ya j...
Comments
Post a Comment